Zanzibar Chamber kupitia mradi wa USAID IMARISHA SEKTA BINAFSI inaendesha mafunzo ya siku tatu kuhusu Utekelezaji wa Rasilimali, Usimamizi wa Fedha na Uhamasishaji wa Wanachama ilikuwajenga uwezo wafanyakazi wa ZNCC kutoka ofisi za Unguja na Pemba. Mafunzo haya yanaratibiwa na Peak Performance International kutoka Dar es Salaam.
Lengo la mafunzo haya ni kuboresha utendaji Kazi wa ZNCC ili kufanikisha malengo yake ya kuihudumia jamii ya wafanyabiashara biashara na kuunganisha sekta binafsi Zanzibar. Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCC, Bw Hamad Hamad , ametoa shukrani zake za dhati kwa Peak Performance International (T) ltd kwa ushirikiano wao usio na kifani kwa ZNCC katika kutoa huduma za mafunzo kwa wafanyakazi wa ZNCC, wanachama wa ZNCC, na jamii kwa ujumla.
Comments